24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Wauaji wa watoto Simiyu wapigiwa kura na wananchi

Na DERICK MILTON

-BARIADI

HATIMAYE zaidi ya wananchi 1,000 wa Kata ya Lamadi, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu,  jana walipiga kura ya siri kuwataja watuhumiwa wa mauaji ya watoto wilayani humo.

 Hatua ilianza saa 5:02 asubuhi na kumalizika saa 7:34 mchana, ambako mamia ya wanawake wakiwa na watoto,   wanaume na vijana walijitokeza kwa wingi kupiga kura.

Upigaji kura huo ulisimamiwa na maofisa wa Usalama wa Taifa kutoka za Wilaya za Itilima, Meatu na Maswa, huku mshangao mkubwa ukiwa ni kutokuwapo   polisi.   

Hata hivyo, Licha ya kukosekana   polisi hatua hiyo ilienda salama hadi kukamilika, huku wananchi, mmoja baada ya mwingine wakipiga kura na kurejea sehemu waliokuwa wamekaa.

  Mtanzania ilipata taarifa kutoka chanzo kimoja (hakikutaka kutajwa jina) kuwa kukosekana kwa  polisi kulitokana na wananchi kulituhumu jeshi hilo wakati wa mkutano wao na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka,  Februari 11.

 Kwenye mkutano huo wananchi  walitaka ipigwe kura baada ya kueleza kutokuwa na  imani na polisi wakidai askari hao wamekuwa wakiwakamata watu wanaotuhumiwa kwa mauaji hayo na baadaye  kuwaachia.

Wakizungumza  baada ya kupiga kura  baadhi ya wananchi walisema wahusika watajulikana tu.

Walimshukuru RC Mtaka kwa kuwakubalia ombi hilo ambalo walieleza ndiyo njia pekee ya kukomesha matukio hayo.

“Tunakupongeza Mkuu wa Mkoa, umeonyesha uongozi wako, umeonyesha kuwatumikia wananchi, hakika tuna kiongozi bora.

“Hii kura ambayo tumepiga hapa inaenda kumaliza tatizo hilo, hofu hapa kwetu imekuwa kubwa,” alisema Alfred Nanai na kuongeza:

 “Hili eneo ni maarufu  hapa Lamadi, matukio yote ya uhalifu na ambayo ni mabaya kwenye jamii yetu yamekuwa yakimalizikia hapa, leo nina miaka 74 hapa ndiyo suluhisho la unyama huu”.

Hata hivyo wananchi hao walimuomba Mtaka kuwaruhusu …

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles