Na TUNU NASSOR
-DAR ES SALAAM
MNYUKANO wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu umeendelea.
Jana mbunge huyo na chama chake cha Chadema wamejibu hoja za waziri huyo juu ya suala la upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwake na uwepo wa CCTV Camera katika eneo lilipotokea.
Lugola alizungumzia mara kadhaa tukio la Lissu ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa Bunge uliopita ambako alisema upelelezi wa tukio hilo unasubiri Lissu arudi nchini.
Hata hivyo, juzi Lugola alienda mbali na kushangaa kwanini Lissu hajakamatwa akidai amekuwa kama mzururaji mwingine, na kwamba anadanganya umma kwamba eneo alipopigiwa risasi kulikuwa na kamera za CCTV na kwamba sasa zimeondolewa.
LISSU
Baada ya maelezo hayo, jana Lissu kupitia moja ya televisheni mtandao, alisema wanaosema harudi nyumbani hakuna hata mmoja aliyeuliza kuhusu hali yake.
 “Wabunge wenzangu wa Chadema wanajua kwa sababu nimekuwa nazungumza nao mara kwa mara na kuwapa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.