28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Watumishi TFS wakumbushwa kutekeleza mujukumu yao kwa weledi

Mwandishi Wetu

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amewataka waajiriwa wapya na wazamani wa TFS kutekeleza majukumu yao kadri sheria za nchi na jinsi maadili yanavyowataka.

Akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha watumishi wapya wa wakala huo, Profesa Silayo amesisitiza suala la uadilifu na maadili katika utumishi kuwa si la mzaha.

“Enendeni mkalitumikie taifa na kamwe msisubiri kufanya kazi kwa kusukumwa, kila mmoja anatakiwa kufanya kazi kwa hiari, kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kuhakikisha utumishi wa umma unaleta tija iliyokusudiwa.

“Nanyi watumishi wa zamani tumewaleta katika mafunzo haya ikiwa ni jitiada za kurejesha uadilifu na maadili miongoni mwenu, ” amesema Profesa Silayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mafunzo ya muda mfupi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Charles Magaya, aliyemwakilisha Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Dk. Emanuel Shindika, ameipongeza TFS kwa kutambua kuwa ili utumishi wa umma uwe wenye ufanisi na wa kuheshimika watumishi wanapaswa kuzifuata Kanuni za Maadili ya Utumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles