23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau wataka viongozi kutumia Kiswahili, waache kupaisha lugha za kigeni

Elizabeth Joachim, Dar es salaam

Wadau wa lugha ya Kiswahili wamesema viongozi wa kitaifa kuzungumza lugha za kigeni katika matukio ya kitaifa ni sawa na kupeperusha bendera za mataifa hayo.

Akizungumza katika warsha ya ufunguzi wa wiki ya tafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tataki) iliyofanyika leo Jumatano Aprili 3, Jijini Dar es Salaam, Mhadhiri wa chuo hicho, Dk. Rajabu Chipila, amesema lugha ya Kiswahili italeta mafanikio ikiwa Watanzania wataona lugha hiyo ni hazina.

“Tunakwama kwa sababu hatuoni Kiswahili ni hazina, kwetu Tanzania Kiswahili ni aibu. Mfumo wetu umeota mizizi kiasi kwamba hata viongozi wakubwa wanaona kuzungumza Kiswahili ndiyo fahari,” amesema Dk. Chipila.

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kuzungumza Kiswahili katika shughuli mbalimbali za kitaifa ni kitendo cha kishujaa na ndiyo wanavyofanya viongozi wa mataifa mengine duniani na kwamba taifa haliwezi kuendelea kwa kuzungumza lugha za mataifa mengine.

“Huwezi kutangaza lugha ambayo huithamini, kwanza ni lazima tuithamini lugha yetu ili tuweze kuitangaza. Mataifa mengi yamefaidika kupitia lugha zao,” amesema Dk. Chipila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles