33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Watuhumiwa kwa kufundisha ngono watoto

MWANDISHI WETU -TUNDURU

WAZAZI 35 kutoka Kata ya Nalasi wilayani Tunduru mkoani Ruvuma,  wamekatwa baada ya kukukutwa wakiwafundisha watoto wa kike walio chini ya umri wa miaka 18  mbinu za kuishi na wanaume na kufanya tendo la ngono maarufu kama msondo.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro ambapo alisema kuwa wazazi hao wamekamatwa  nyakati za usiku wakiwa wamejifungia kwenye nyumba mmoja wa waliokamatwa katika Kijiji cha Nalasi wakiwa na watoto hao.

Alisema, wazazi hao wamekamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema kwamba, kuna wazazi  wamewaficha watoto wa kike wenye umri mdogo na kuwafundisha mila potofu zinazohusiana na mambo ya ngono ambayo hayapaswi kufundishwa watoto wadogo.

Mtatiro alisema, wazazi hao walikamatwa nyakati za usiku wakiwa na watoto hao wadogo  wakiwa katika moja ya nyumba iliyokuwa inatumika  kwa shughuli hiyo.

Pia alisema, katika msako huo mbali na wazazi hao wamemkamata kungwi mmoja, mtendaji wa kijiji, Rajabu Lusanga na mwenyekiti wake Ali Omari ambao wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya wazazi hao licha ya kuishi jirani na eneo la tukio hilo.

Kwa mujibu wake shughuli za msondo hazikatwi kufanywa, isipokuwa ni kwa wasichana wakubwa wenye umri zaidi ya miaka 18 na wale wanatarajia kuolewa, badala ya kuwafundisha watoto wadogo ambao hawana uwezo wa  kuelewa jambo lolote.

“Natoa wito kwa wazazi wote katika Wilaya ya Tunduru tabia ya kuwafundisha watoto wadogo namna ya kuishi mama na baba jambo hilo tumelipiga marufuku kwani linachangia sana kuongezeka kwa mimba na wasichana wengi kuacha shule,” alisema Mtatiro.

Alisema, vitendo hivyo vinasababisha watoto wadogo wa kike kukosa haki yao ya kupata elimu na kusisitiza kuwa operesheni hiyo itaendelea katika vijiji mbalimbali hadi pale jamii itakapo acha kufanya vitendo hivyo.

Baadhi ya wakazi wa Tunduru wamepongeza jitihada kubwa zinazo fanywa na Serikali ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya kukomesha baadhi ya mira potofu ambazo zimekuwa chanzo cha kuongezeka kwa mimba kwa watoto wa kike wengine  kuacha masomo.

Ali Shaibu mkazi wa Nakayaya alisema kuw jitihada zinazofanywa na mkuu wa wilaya zinapaswa kuungwa mkono na jamii ya watu wa Tunduru kwani zitasaidia kuepusha mimba za utotoni,kupata  magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na kupoteza vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya familia na Taifa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles