33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mamia wajitokeza maonesho ya Sabasaba

CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Dk. Ng’wanza Soko  amesema licha ya nchi kupitia kipindi kigumu hivi karibuni cha  ugonjwa wa Corona Covid 19, idadi ya wananchi waliotembelea  Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba mwaka huu katika sherehe za Sabasaba imeongezeka kutoka  53,456 mwaka jana na kufikia 57, 608 mwaka huu.

Akizungumza jana wakati wa  hafla ya ufungaji Maonyesho  ya Biashara ya 44 ya Sabasaba , Soko alisema idadi hiyo ni ya wananchi waliotembelea siku ya Julai 7, mwaka huu yaani kilele.

“Mbali ya kupitia changamoto mbalimbali za ugonjwa wa Corona Covid 19 na idadi ya washiriki kupungua lakini wananchi waliotembelea katika maonyesho haya hasa siku ya Julai 7, imeongezeka zaidi ya 4,000   tofauti na waliotembelea mwaka jana hivyo maonyesho yamekuwa mazuri zaidi,” alisema Soko.

Alisema Tantrade itaendelea kufanya maboresho mbalimbali ili kuhakikisha maonyesho hayo mwakani yanakuwa mazuri zaidi.

Alisema maonyesho hayo ni muhimu kwa sababu yana Kumbukumbu ndani ya nchi ambayo ni ya kuzaliwa kwa chama cha Tanganyika National Union (TANU),

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Riziki Shemdoe alisema Serikali inaendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo ndani na nje ya nchi ili kupata masoko ya uhakika.

Alisema wamefarijika kutembelewa na wafanyabiashara, wanafunzi, mashirika ,taasisi mbalimbali na kupokea maoni mbalimbali ambapo baadhi ya maoni hayo.kuendleea kuimarisha kwa mifumo hiyo, kuhamasisha makundi mbalimbali kushiriki ili kutangaza fursa na wananchi kujifunza.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali alisema matumizi ya teknolojia, ubinifu, rasilimali watu na utafiti vinasaidia kukuza uchumi viwanda na ajira endelevu nchini

Alisema baada ya benki ya dunia kuitangaza Tanzania imefikia uchumi wa kati na kuona juhudi zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kunahitajika nguvu ya pamoja katika utendaji kazi.

Alisema Tanzania imeingia kwenye kundi la uchumi wa kati kama ambavyo nchi za Asia zilivyokuwa zikijivunia na kunahitajika teknolojia za kisasa  kurahisisha utendaji kazi.

Aliongeza kuwa nchi yenye viwanda inahitaji nguvu kazi ya wananchi wake ili iweze kuzalisha bidhaa zake zenye ubora na zitakazokuwa zinanunuliwa ndani na nje ya nchi. 

Balozi Amina,  alisema ili kuendana na kauli mbiu ya maonesho hayo, wanapaswa kuuunganisha mazao katika mnyonyororo wa thamani ili kupata masoko zaidi nje ya nchi. 

Alisema sekta binafsi zinapaswa kushirikiana na serikali ili kukuza uchumi wa kati juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles