WATU 18 WAJERUHIWA AJALINI DAR

0
906
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni

NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM

WATU 18 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea saa 10:30 alfajiri katika eneo la Madafu barabara ya Pugu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani alisema ajali hiyo ilihusisha  gari  namba T 337  BKN Nissan Civilian iliyokuwa inatoka Gongo la Mboto – Mombasa kwenda Kariakoo kupitia Banana.

“Gari hilo liliigonga gari  la mchanga namba T 656 DHL Scania 94   lililokuwa likitokea Banana kwenda Gongo la Mboto,.

“Watu 18 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Amana wakati wengine walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).  Hali za  majeruhi watatu   zilikuwa mbaya,” alisema.

Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha hospitali hiyo   ilipokea majeruhi tisa na mwili mmoja wa marehemu.

Mwangomo aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kuwa ni  Masiku Werema (45), Mohamed Juma (37), Adam Rashid (25) na Joshua Stephen (32).

Wengine ni Said Juma (17), Eliza Chacha (14), Maua Malick (48), Stella Mpahe (35) na Juma Mtally.

“Kati ya majeruhi hao, Adam Rashid alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kutengamaa,” alisema.

Mwangomo alisema majeruhi wengine bado wamelazwa  wakiendelea kupatiwa matibabu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here