HALIMA MDEE AKAMATWA KWA AGIZO LA DC

0
681
MBUNGE Kawe, Halima Mdee (Chadema)

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


MBUNGE Kawe, Halima Mdee (Chadema), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kutokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.

Mdee alikamatwa jana nyumbani kwake Makongo na kuepekwa katika kituo cha Polisi Oysterbay, ambapo taarifa za kukamatwa kwake aliandika katika moja ya magrupu ya WhatApp jana jioni.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, aliliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kumkamata Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), kwa kile kilichodaiwa kuwa alitoa kauli za uchochezi na matusi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Alisema Mdee anatakiwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 48 kisha ahojiwe na kuchukuliwa hatua za  sheria kuhusu maneno aliyoyatoa juzi  alipozungumza na waandishi wa habari, akiwa makao makuu ya Chadema.

Alitaja kauli alizosema ni za uchochezi na zilitolewa na Mdee kuwa ni pamoja na kusema Rais Dk. Magufuli ana tabia ya ovyo.

“Katika mazungumzo yake, Mdee alisema ipo siku Rais ataagiza Watanzania tutembee vifua wazi wanaume kwa wanawake, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na misingi ya dini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here