25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

WATOTO 500 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NDANI YA MIAKA MIWILI

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

WATOTO 570 wamefanyiwa upasuaji wa kutibu magonjwa ya moyo tangu mwaka 2015 hadi hivi sasa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa Taasisi hiyo, Naiz Majani, alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kambi ya matibabu dhidi ya magonjwa ya moyo kwa watoto ambayo inafanywa na JKCI kwa kushirikiana na Shirika la Marekani la Mending Kids International.

“Kati ya watoto hao, 360 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya bila kufungua kifua na watoto 218 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya kufungua kifua,” alisema.

Alisema idadi ya watoto wanaofanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo imeongezeka na imekuwa ikifanyika kwa mafanikio ikilinganishwa na awali huduma hiyo ilivyoanza kutolewa nchini.

“Huduma za matibabu ya moyo nchini zilianza rasmi kutolewa mwaka 2008 ambapo kwa upande wa watoto tuliweza kuwafanyia upasuaji 200 tu hadi tunafikia mwaka 2015 (kwa kipindi cha miaka minane.

“Lakini utaona baada ya Taasisi kuanza na kutenga kitengo maalumu kwa ajili ya watoto idadi imeongezeka na wengi tumeokoa maisha yao, kwa mwaka Serikali ilikuwa na uwezo wa kupeleka watoto kati ya 40 hadi 80 kwa mwaka kwenda kutibiwa magonjwa haya nje ya nchi.

“Kwa hiyo tunajivunia kwamba huduma zinazidi kuimarika na tunazidi kuokoa maisha ya wengi ambao tungewapoteza kutokana na magonjwa haya,” alisema.

Kuhusu upasuaji unaoendelea, Dk. Naiz, alisema hadi kufikia jana jumla ya watoto 28 walikuwa wamefanyiwa upasuaji mkubwa na mdogo kutibu magonjwa hayo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles