22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Watanzania watakiwa kutumia nishati mbadala ili kutunza mazingira

Na Mwandishi Wetu, Moshi

Katika kutokomeza uharibifu wa mazingira nchini, Watanzania wametakiwa kutumia nishati mbadala ya umeme hali itakayosaidia kutunza mazingira na kuhifadhi uoto wa hasili.

Akizungumza Mei 9, mwaka huu katika kikao cha pamoja na wadau wa maendeleo, wakati akitambulisha mradi mpya wa jiko linalotumia nishati ndogo ya umeme, Afisa Biashara wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na nishati na mazingira TaTEDO, Dora urio, amewataka wananchi kutumia nishati mbadala ya umeme ili kuweza kuondokana na ukataji miti ovyo kutoka na asilimia kubwa ya watu wanaotumia nishati ya kuni na mkaa.

Urio amesema katika tafiti iliyofanya na shirika hilo asimia 92 ya watanzania wanatumia nishati ya kuni na mkaa huku asilimia 8 pekee wakitumia nishati ya umeme na gesi,

“TaTEDO imekuja na jiko jipya linalaotumia nishati ndogo ya umeme ambapo mtanzania anaweza kutumia chini ya Sh 200 kupika Maharagwe”alisema Dora

Mmoja wa washiriki, Mchungaji Joselin Njama, alisema majiko hayo banifu yanasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira uliopitiliza, hususani ukataji miti ovyo.

Amesema jamii ya kitanzania imezoea kutumia nishati ya mkaa na kuni kwa ajili, ya kupikia na kuwataka wadau wa mazingira kujikita kutoa elimu juu ya utumiaji wa nishati mbadala.

Kwa upande wake mtaalam wa mazingira manispaa ya Moshi, Emmanuel John amesema suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira unaendana na matumizi ya nishati Mbadala ya umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles