27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Walinda amani 120 wa UNAMID wanatafuta hifadhi Sudan

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), pia lilithibitisha kwamba walinda amani hao wa zamani wameomba hifadhi huko nchini Sudan

Walinda amani wa zamani takribani 120 kutoka Ethiopia mahala ambapo mikoa kadhaa ikiwemo wa kasakzini wa Tigray imeathiriwa sana na mzozo wa kikabila, wanatafuta hifadhi nchini Sudan, Umoja wa Mataifa umesema Jumapili.

Wafanyakazi walipangiwa kurudishwa nyumbani kama sehemu ya kuondoka kwa awamu kwa tume hiyo ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa (UNAMID) kutoka mkoa wa Darfur magharibi mwa Sudan baada ya mamlaka yake kumalizika Disemba 31.

“Kufikia sasa walinda amani 120 wa zamani wa UNAMID ambao walilazimika kurudishwa wameomba ulinzi wa kimataifa,” msemaji wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa, aliliambia shirika la habari la AFP kupitia barua pepe.

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), pia lilithibitisha kwamba walinda amani hao wa zamani wameomba hifadhi nchini Suda

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles