29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

WATANZANIA WALIOSHIKILIWA MALAWI WAACHIWA

MZUZU, MALAWI


HATIMAYE Watanzania wanane waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ujasusi nchini Malawi wameachiwa huru.

Watanzania hao, waliachiwa baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikiwakabili, iliyotolewa hukumu juzi jioni na kuonekana hawana hatia.

Walikuwa wanashikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani uliopo eneo la Kayerekera.

Serikali ya Tanzania ilikataa kwamba Watanzania hao walitumwa ili kufanya shughuli za kijasusi katika mgodi huo.

Ilisema kuwa walikuwa wafanyakazi wa Taasisi ya Misaada ya Caritas iliyo chini ya Kanisa Katoliki, Jimbo la Songea mkoani Ruvuma.

Wakili aliyekuwa anawatetea katika kesi hiyo, Flaviana Charles, alisema wateja wake wameachwa huru ingawa wamepitia wakati magumu mengi.

“Wamepitia wakati mgumu na mambo mengi ya kukatisha tamaa, kila kitu kilikuwa wazi na upande wa walalamikaji hawakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwafunga kwa sababu waliingia Malawi kihalali kuanzia mpakani na walikuwa na mwaliko,” alisema.

Alisema wakati wanawakamata walikuwa hawajafika mgodini, kwa sababu walikuwa hotelini walikokuwa wamefikia.

Wakili Flaviana, alisema kuna ujanja ambao mahakama iliutumia ili kukwepa fidia kwa kudai tayari wametumikia kifungo kipindi hicho chote walichokuwa wameshikiliwa.

Watanzania hao, walishikiliwa kwa muda wa miezi mitatu bila kujua kinachoendelea katika familia zao na shughuli zao za kila siku.

Walisema walikuwa wakiteseka bila sababu wakati nia yao ya kwenda Malawi ilikuwa njema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles