27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Watanzania Milioni 7 wana matatizo ya akili, Dar kinara

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

IMEELEZWA zaidi ya Watanzania milioni 7 wana matatizo ya afya ya akili huku Mkoa wa Dar es Salaam ukitajwa kuwa kinara kwa kuwa na watu wengi wenye tatizo hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Oktoba 9, 2021 jijini Dodoma, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili duniani, Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Shadrack Makubi amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha Watanzania milioni 7 wana matatizo ya afya ya akili.

Alipoulizwa ni Mkoa gani ni kinara wa tatizo hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo ameutaja Mkoa wa Dar es Salaam kuwa unaongoza kutokana na watu wenye matatizo kwenda Jijini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya magonjwa ya akili, Dk. Innocent Mwambeki amesema vyanzo vya ugonjwa wa afya ya akili ni mama mjamzito kutumia vilevihatua inayoathiri ukuaji wa mtoto pamoja na  ukuaji wa ubongo, ukatili kwa watoto, unyanyasaji, vinasaba katika ukoo, umaskini, matatizo kazini.

“Kuna magonjwa ya akili yapo ndani kwa ndani kama Sonona na wasiwasi  hili la vinasaba linatoka katika ukoo na mtu wa namna hii akitumia kilevi mfano Bangi anaripuka moja kwa moja,”amesema.

Amesema watu zaidi ya milioni 300 wana matatizo ya afya ya akili duniani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe, Dk. Paul Lawale amesema wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya hospitali hiyo kuwa chakavu kutokana na kujengwa miaka 95 iliyopita.

Amesema Hospitali hiyo inahitaji uwekezaji zaidi kwani kwa sasa wanauwezo wa kuhudumia wagonjwa 590 wakati waliopo kwa sasa ni 400

“Pia tuna changamoto ya kuwarejesha katika jamii wagonjwa wanapopata nafuu, tunajua wanatoka Mikoa mbalimbali sasa wanapopata nafuu ndugu huwa hawaonekani hivyo tunakutana na wakati mgumu,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles