29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Guseni wananchi kihuduma’-Dk. Mpango

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango amelitaka Shirika la Posta Tanzania kugusa jamii kihuduma kwakuwa ilianzishwa ili kuhakikisha linatoa huduma kwa niaba ya Serikali na kuwahudumia wananchi wote bila kujali mahali walipo.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 9, 2021 wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Posta Duniani ambapo, amelitaka shirika hilo, liguse jamii kihuduma kwakuwa ilianzishwa ili kuhakikisha inatoa huduma kwa niaba ya serikali na kuwahudumia wananchi wote bila kujali mahali walipo.

 “Tumeshuhudia mageuzi makubwa ndani ya Shirika letu la Posta, mmeleta huduma mbalimbali zinazoakisi matumizi ya teknolojia katika kuwahudumia Watanzania. Nawapongeza sana kwa hayo.Ninafurahi kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya malengo makuu ya Umoja wa Posta Duniani na malengo yetu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na yale ya Sera ya Taifa ya Posta ya 2003 hasa katika kuwahudumia wananchi,”amesema Dk. Mpango.

Amesema wameshuhudia Posta ikibadilisha namna ya utoaji huduma zake kwa jamii kulingana na mahitaji na ndio maana wanashuhudia Posta kuwa ya kidigitali na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi kwa urahisi.

“Tunahitaji kuwa na utendaji wenye tija ikiwa ni pamoja na kutumia mtandao mpana wa Shirika la Posta ambao una matawi zaidi ya 350 yaliyosambaa nchi nzima, bara na visiwani,” Dk. Mpango.

Amesema Umoja wa Posta duniani ni chombo cha Umoja wa Mataifa (UN) chenye jukumu la kuendeleza huduma za Posta hapa duniani.

“Katika mkutano mkuu wa Umoja wa Posta Duniani Tanzania iifanikiwa kushika nyadhfa za uongozi kwenye viti vya ujumbe katika mabaraza yote mawili ya umoja huo, yani Baraza la Utawala (Council of Administration) na Baraza la uendeshaji la Posta (Postal Operations Council),”amesema.

Amesema wamefanya maadhimisho haya kwa siku nne mfululizo na kushirikisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Posta na nje ya Sekta ya Posta,ambapo amedai  nia ni kuonesha umma umuhimu wa huduma za Posta nchini.

Naye, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rahma Kassim Ali amesema wanatoa hongera kwa umoja wa Posta duniani kwa kufikisha miaka 147 tangu kuanzishwa kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles