29.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

‘Watanzania 66 katika kila 100 hawana bima ya afya’

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

WATANZANIA 66 katika kila 100 hawana bima ya afya na hulazimika kulipia huduma za matibabu kwa pesa taslimu, pindi wanapougua jambo linaloelezwa kwamba linaongeza hatari ya kukosa matibabu pindi wanapougua na hawana fedha mfukoni.

Hayo alisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Health Promotion Tanzania (HDT), Salvatory Hokororo, katika maadhimisho ya siku ya afya duniani iliyoadhimishwa Aprili 6 ya kila mwaka.

Alisema mpango mkakati wa kugharimia afya ulioundwa mwaka 2015 uliazimia kuunda mfuko wa bima ya afya kwa wote na mfuko mmoja wa kuwekeza fedha kwa ajili ya afya ili kuondoa matumizi makubwa kwenye huduma ya afya yanayoweza kuleta kifo.

“Mkakati huu mpaka mwezi uliopita wakati wa wiki ya sera ya afya ulikuwa bado haujaidhinishwa. Bajeti ya sekta ya afya siyo tu ni nusu ya mahitaji bali hata zinazotolewa huwa ni pungufu huwa ni pungufu ya bajeti iliyotengwa. Mfano mwaka 2017/18 makadirio yalikuwa ni Shilingi Trilioni 4.35 wakati bajeti ilikuwa Shilingi Trilioni 2.2.

“Kutokana na hali hii matokeo yake, Tanzania haijafikia malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) 3.8.1 inayoeleza kuongeza huduma za afya muhimu, ambapo ni watu 36 kati ya 100 wanapata huduma muhimu za afya ukilinganisha na asilimia 57 kwa nchi ya Kenya, asilimia 53 kwa Rwanda na asilimia 44 kwa Uganda,” alisema Hokororo

Alisema wakati Tanzania inaungana na harakati za kimataifa kuhakikisha kila mtu ambaye anahitaji matibabu anapata bila kizuizi cha fedha.

“Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Dk. Tedros Adhanom katika kuadhimisha siku hii alisema kwamba; afya ni haki ya binadamu. Hakuna mtu anapaswa kuumwa na kufa kwa sababu ni masikini au kwa sababu hawezi kupata huduma za afya anazohitaji.

“…je lini kwa viongozi wetu wa kisiasa au serikali wanasema maneno haya? Tunatoa wito kwa viongozi kuamua kwa dhati juu ya afya kwa wote na kuwekeza katika afya kwa wote,” alisema Hokororo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles