25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Ronaldo awapa matumaini Juventus

TURIN, ITALIA 

KOCHA wa Juventus, Massimiliano Allegri, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo juu ya hali ya mshambuliaji wao, Cristiano Ronaldo, kwa madai atakuwa fiti kuwavaa wapinzani wao Ajax kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa keshokutwa.

Mchezaji huyo juzi alikuwa benchi katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AC Milan, hata hivyo amekuwa nje ya uwanja na kukosa michezo mitatu tangu alipopata tatizo la nyama za paja wakati anaitumikia timu ya taifa Ureno.

“Ronaldo sasa yupo tayari, lakini katika mchezo wa leo (juzi), nilimwambia anatakiwa kupumzika kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ajax, hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi,” alisema kocha wa timu hiyo, Allegri.

Mchezaji huyo amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Juventus kutinga hatua ya robo fainali. Aliifikisha timu hapo baada ya kufunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Atletico Madrid, baada ya mchezo wa awali Juventus kukubali kichapo cha mabao 2-0.

Hivyo, kuumia kwake kuliwapa wasiwasi mashabiki wengi juu ya kuwavaa Ajax ambao wameonesha ushindani mkubwa kwenye michuano hiyo baada ya kuonesha ubora wao na kuwaondoa waliokuwa mabingwa watetezi Real Madrid.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles