23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wasimamizi uchaguzi wafundwa, waonywa

Na MURUGWA THOMAS-TABORA.

WARATIBU wa uchaguzi wa mikoa na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Wilaya na majimbo wameonywa kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kutakiwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi.

Akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasimamizi hao wa uchaguzi 110 toka mikoa na wilaya za mikoa ya Kigoma na Tabora ofisa sheria wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Athuman Kihamia ameonya kwamba watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria.

Kihamia amesema lengo la kutoa mafunzo hayo kwa waratibu na wasimamizi ni kutaka wasimamie Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu uwe huru, wa haki na kuaminika.

Amewataka wazingatie viapo vyao kwani vinawataka watende majukumu yao kwa mujibu wa sheria na endapo watakiuka watakuwa wametenda kosa la jinai hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za uchaguzi zinavyoelekeza.

Kihamia amebainisha kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi inao wajibu wa kutoa mafunzo yanayolenga taratibu za kuendesha uchaguzi kwa waratibu wa mikoa, wasimamizi wa ngazi zote wakiwemo wa wilaya, majimbo,vituo pamoja na maofisa ugavi.

Akifungua mafunzo hayo, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, (NEC) Hassan Mwandobo alisema kuwa mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi.

Mwandobo amewataka washiriki wa mafunzo hayo watambue kuwa wameaminiwa kufanya kazi hiyo, hivyo ni muhimu wakajiamini na kutambua kwamba wanapaswa kuzingatia kanuni za uchaguzi, maadili yake na maelekezo yatakayotolewa na Tume.

Amewataka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao wavishirikishe vyama vya siasa pamoja na wadau wengine wakiwamo viongozi wa dini.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora Isike Mwanakiyungi mjini hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles