25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WASANII WASAIDIWE KUZIFIKIA DILI ZA KIMATAIFA


WAKATI Tanzania habari kubwa ikiwa ni wasanii kufungiwa kazi zao, tunamshuhudia rapa wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest akinyakuwa dili nono kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ikiwa ni saa chache baada ya kuachia video ya wimbo Check On You, aliomshirikisha Davido  ambao kwa hali ya sasa kimaudhui sidhanai kama runinga zetu zinaweza kuucheza.

Cassper Nyovest amekuwa kwenye orodha ya wasanii wakubwa Afrika ambao wanapata dili nono za kimataifa zinazomwingizia kipato kikubwa nje ya kazi yake ya muziki.

Ikumbukwe kuwa rapa huyo  hapa Afrika ni balozi wa kinywaji cha Ciroc ambacho kinamilikiwa na Sean Combs ‘ P Diddy’ wa Marekani na mara zote amekuwa ni mlipaji mzuri wa kodi nchini mwao.

Kwa hapa   Bongo bado hali ni tete. Wasanii wanalazimika kutumia nguvu zao binafsi kutafuta kolabo  za kimataifa ambazo tunatarajia ziwakutanishe na kampuni kubwa zitakazowapa dili  ila wanakutana na suala la ‘maadili’ wanajikuta wanarudi nyuma.

Binafsi natamani kuona Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiweka hadharani mikakati yake ya kuhakikisha kwa mwaka fulani, wasanii kadhaa wawe wamepata dili kubwa za kibalozi kwenye kampuni za kimataifa.

Natamani kuona, Wizara yetu inakuwa mstari wa mbele kuwaunganisha wasanii wetu na wale wa kimataifa ambao ni ngumu kuwapata kwa njia binafsi ili wafanye nao kazi lengo likiwa ni kutanua muziki wetu.

Kwa sababu msanii anapofanikiwa hulipa kodi, atengeneza ajira kwa vijana wengine na kufanya kiwanda cha burudani kikue kwa kasi hasa kipindi hiki kuelekea Tanzania mpya ya viwanda.

Tunaona Diamond anavyojitahidi kuonyesha namna msanii akisimamiwa vizuri anavyoweza kuwa na tija kwenye nchi. Tunapofurahia mafanikio ya Chibu tufikiria kuwatengeneza kina Diamond wengine.

Na njia ni moja tu ya kuwapa ushirikiano na uhuru wa kufanya kazi zao bila kuwawekea mipaka. Sitaki kuamini kama tatizo ni hili moja tu la wasanii kuvunja maadili.

Kuna matatizo lukuki ambayo yanawakwamisha wasanii kibishara kwenye anga la kimataifa kama wanavyopata wasanii wa mataifa mengine. Tutatue matatizo hayo tukimaliza hili la maadili na wahusika wawe mstari wa mbele kutengeneza njia za wasanii wetu kutazamwa kwa jicho la kibiashara na mataifa mengine.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles