28.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Wasanii kunufaika na viwanja vya mkopo

Brighiter Masaki, Dar es Salam

Kampuni ya KC Land Development Plan imepanga kuwapatia wasanii ambao ni wanachama wa kikundi cha Uzalendo Kwanza viwanja kwa mkopo ili waweze kumiliki ardhi na kujenga makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 2, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Steve Magere maarufu Steve Nyerere amesema kampuni hiyo imefanya jambo kubwa na muhimu kwa wasanii.

“Wasanii tumekuwa tukitangatanga katika nyumba za kupanga tunawashukuru KC kwa kutuona na kutuwezesha kupata ardhi kwa kuwa heshima ni kuwa na nyumba na si gari, kama ilivyo kaulimbiu yetu kwamba “Maisha ni nyumba” amesema Nyerere.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa KC, Halid Mwinyi amesema wamejipanga kuwainua wasanii na wananchi kwa kuwapa viwanja kwa bei nafuu.

“Tumeanza na wasanii baada ya hapo tutafata makundi mengine kwa mkopo ambao hauna riba viwanja hivyo vipo eneo la Kigamboni na Kibaha” anasema Mwinyi.

Aidha wasanii watakutana na kampuni hiyo Mei 5 kwa kwa ajili ya kuingia mikataba na kupeana maelekezo ya namna ya kufanikisha zoezi hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,908FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles