23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wanunuzi wa madini wazindua chama chao wakitaja changamoto inayowatesa

Na Clara Matimo, Mwanza

Chama cha Mabroka wa Madini Tanzania (Chammata) kimezindua rasmi chama chao ambacho lengo kuu ni kuwaunganisha, kuwasimamia na kutetea maslahi ya wafanyabiashara wadogo wa madini huku kikitaja changamoto ya ufanyaji biashara kwa kuwa na leseni kila mkoa ni  kikwazo katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija.

Uzinduzi huo umefanyika Julai 13 jijini Mwanza ukihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, aliyemwakilishwa Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko,

Mwenyekiti wa Chammata, Jeremia Kituyo, alisema kulazimika kuwa na leseni kila mkoa wanaofanya biashara  inawaumiza kiuchumi huku akiiomba Serikali kuweka utaratibu wa upatikanaji  leseni kikanda, ili kuwarahisishia shughuli za uchimbaji wafanyabiashara wadogo wa madini.

“Kwa sasa leseni zinakatwa kimkoa, ikimaanisha kwamba mchimbaji awe na idadi ya leseni kutokana na idadi ya mikoa anayohitaji kununua madini. Kama ni mikoa 25 anayotaka kununua madini, kwa mfano, ni lazima awe na idadi hiyo ya leseni na muombaji atalazimika pia kutembelea ofisi 25 za mamlaka ya mapato,” alifafanua Kituyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, aliyemwakilisha Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko, (katikati) akiwa amenyenyua cheti cha Chammata ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa chama hicho uliofanyika Julai 13, 2022 jijini Mwanza,(kushoto) ni Mwenyekiti wao, Jeremia Kituyo, (kulia) ni Kamishina wa Madini Mkoani humo, Nyaisara Mgaya.

Alisema hatua hiyo ni kwamba mbali na kupoteza muda, gharama zinakua kubwa kwani kila leseni inalipiwa Sh 250,000 ambapo chama hicho kimejidhatiti kuwa na mchango mkubwa  katika kuchangia ukuaji wa pato la taifa kupitia sekta ya madini, ikiwemo kuthibiti utoroshwaji wa madini pamoja na kuwaunganisha madalali ili kuzuia uuzaji holela wa madini,” alisema mwenyekiti huyo.

Hata hivyo akitolea ufafanuzi juu ya changamoto hiyo iliyowasilishwa na wanunuzi hao, Waziri wa Madini, Dk. Biteko kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Gabriel, alisema suala hilo linaendelea kutafutiwa ufumbuzi huku akiwapa matumaini kuwa baadhi ya changamoto walizoziwasilisha katika mkuatano wa awali jijini Arusha zimeishaanza kufanyiwa kazi.

“Kwa kuwa Serikali yenu ni sikivu hadi sasa kuna changamoto ambazo
zilielezwa katika kikao hicho zimefanyiwa kazi. Hata hivyo, baadhi ya changamoto ikiwemo ufanyaji wa biashara kwa mikoa yote kwa kutumia leseni moja, pamoja na vipengele kwenye mwongozo wa biashara ya madini vinaendelea kutafutiwa ufumbuzi na wizara. Mbali na juhudi zote za chama chenu Serikali inawapongeza kukamilisha usajili kamili na sasa mnatambulika rasmi katika Serikali,” alisema Biteko kupitia hotuba yake.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (Femata), Lister Balegele, aliiambia Mtanzania Digital kwamba uanzishaji wa Chammata utawarahisishia wachimbaji  uuzaji wa madini kwenye migodi kwani broka ni kiunganishiki kati ya mchimbaji mdogo na mnunuzi mkubwa wa rasilimali hiyo(dila).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles