Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
KAMPUNI ya Geita Gold Mine Limited (GGML), imeendelea kung’ara baada ya kuibuka mshindi katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara – Dar es Salaam maarufu kama sabasaba kwa kunyakua tuzo ya muajiri bora na msafirishaji bora wa madini nje ya nchi.

Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji.
Pia GGML imepata tuzo ya mlipa kodi bora wa pili na muajiri bora anayezingatia taratibu za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
