29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Katibu Mkuu ACT aongoza ujumbe wa chama hicho kuzungumza na DC Jokate

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Ado akiambatana na Katibu wa Fedha na Miradi, Rachel Kimambo, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Renatus Pamba na Mwenyekiti wa Jimbo la Mbagala, Muhdeen Mkwera wamemtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Jokate Mwegelo kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Ujumbe wa ACT Wazalendo ukiongozwa na Katibu Mkuu, Ado Shaibu Ado wapili kutoka kushoto, ukiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Jokate Mwegelo(Katikati).

Akitambulisha malengo ya ziara hiyo,leo Alhamisi Julai 14, 2022, Ado amesema amemtembelea Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kubadilishana naye mawazo kuhusu changamoto mbalimbali za Wananchi zilizopatikana kwenye ziara ya Katibu Mkuu kwenye Jimbo la Mbagala kuanzia Juni 29 hadi Julai 6, mwaka huu.

“Kaulimbiu ya ACT Wazalendo ni Taifa Kwanza leo na kesho. ACT Wazalendo tumeshakutana na Mh. Rais Samia Suluhu juu ya masuala mbalimbali ya Mwelekeo wa Nchi kisiasa. Leo, nimewaleta viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

“Binafsi ninaamini kuwa tunao wajibu wa kubadilisha siasa za Nchi kwenda kwenye siasa za mkazo wa masuala ya Wananchi. Hili linahitaji ushirikiano wa karibu na viongozi wa Serikali katika kubadilishana mawazo na Taarifa,” amesema Ado.

Akijibu hoja zilizoibuliwa, Jokate amemshukuru Katibu Mkuu Ado kwa kumtembelea na kuziwasilisha changamoto hizo kwake na kumhakikishia kuwa changamoto zilizowasilishwa kuhusu masuala ya barabara, afya, wamachinga na bodaboda zinaendelea kufanyiwa kazi na Serikali.

“Kuhusu barabara ya Nzasa-Kilungule-Buza, nilifanya mazungumzo na mkandarasi. Ameshalipwa. Ni matumaini yangu kuwa itakamilishwa kwa wakati. Pia, tunatarajia kupata awamu nyingine ya mradi wa DMDP ambao utaneemesha barabara nyingi mlizozilalamikia,” amesema Jokate.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Ado Shaibu amemhakikishia DC Jokate kuwa Chama cha ACT Wazalendo kinashiriki na kitaendelea kushiriki ipasavyo kwenye kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi kwa sababu ni suala muhimu kwa ustawi wa Taifa letu kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles