25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Wanne wafariki kwa homa ya Dengue

Ramadhan Hassan-Dodoma

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto imesema mpaka sasa watu wanne wamefariki kutokana na Homa ya Ugonjwa wa Dengue.

Akitoa kauli ya Serikali bungeni leo June 21, Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu amesema kwamba jumla ya watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa huyo ambapo kwa Mkoa wa Dar es salaaa wamefariki watu watatu na Dodoma mmoja.

Waziri Ummy amesema jumla ya wagonjwa 4,320 na vifo 4 vimetolewa taarifa huku Mkoa wa Dar es salaam ndio ukiwa kinara kwa kuwa na wagonjwa wengi.

“Mkoa wa Dar e salaam una wagonjwa 4,029 na vifo vitatu, Dodoma wagonjwa watatu na kifo kimoja, Tanga wagonjwa 207 kifo hakuna, Pwani 57 hakuna kifo, Morogoro 16 hakuna kifo, Arusha watatu hakuna kifo, Singida wawili hakuna kifo, na Kagera wawili hakuna kifo,” amesema.

Aidha amesema kuwa takwimu za hali ya maambukizi ya ugonjwa wa Dengue zinaonesha kuwa maambukizi mapya yamepungua kutoka wagonjwa 2494 kwa mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 813 kufikia tarehe 19 Juni 2019. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles