27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Baba amjibu Rihanna

NEW YORK, MAREKANI

MAPEMA mwaka huu, msanii wa muziki wa pop, Rihanna Fenty, alitangaza kumchukulia hatua baba yake Ronald Fenty kutokana na kutumia jina la Fenty katika biashara zake.

Rihanna alidai kuwa baba yake huyo amekuwa akitumia jina hilo wakati anajua kama yeye analitumia kwenye biashara yake ya vipodozi, hivyo alidai mzazi wake huyo ananufaika kupitia ustaa wa Rihanna.

Baada ya kimya kirefu, mzee huyo ameamua kuweka wazi kuwa, alianza kutumia jina hilo kabla ya Rihanna kuanza kuwa maarufu.

“Nimekuwa nikitumia jina la Fenty kwenye biashara zangu kabla ya Rihanna, nilishangaa kuona anakuja juu, nadhani ameamua kufanya hivyo kwa kuwa sasa jina lake limekuwa kubwa na anafanya vizuri kwenye bidhaa zake, lakini ukweli ni kwamba nilikuwa wakwanza kufanya biashara kabla yake,” alisema baba wa Rihanna.

Wiki kadhaa zilizopita Rihanna alitajwa kuongoza kwa utajiri kwa upande wa wasanii wa kike huku akiwafunika Beyonce, Madonna na wengine wengi kutokana na biashara zake za vipodozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles