25.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake WHI watoa msaada Hospitali ya Ocean Road

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Machi 8, kila mwaka Wanawake kote duniani huungana kuadhimisha SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake 2024 inasema; Wekeza kwa wanawake kuharakisha maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii.

Wanawake wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakiwa katika picha ya pamoja.

Hapa nchini katika kuadhimisha siku hiyo Wanawake wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wametoa msaada wa dawa na mahitaji muhimu kwa ajili ya wagonjwa wa saratani katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi Msaada huo Afisa Utumishi Mkuu wa WHI, Priscila Ambelile amesema msaada huo ni sehemu ya kusherehekea siku ya Wanawake duniani huku wakitambua kazi kubwa inayofanywa na Taasisi hiyo ya Ocean Road.

Afisa Utumishi Mkuu wa WHI, Priscila Ambelile(kulia) akikabidhi msaada huo kwa Uongozi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

“Kama inavyofahamika kwamba leo Machi 8, 2024 tunaadhilisha Siku ya Wanawake Duniani nasisi wanawake wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment(WHI) tumeona tuadhimishe siku hii kwa kuikumbuka.

“Hivyo tumekabidhi msaada wa dawa na mahitajki mengine kwa Taasisi hii ya Ocean Road jijini Dar es Salaam tukijua kabisa kuwa utaenda kusaidia Wanawake wenzetu na Watanzania kwa ujumla wanaosumbuliwa na ugonjwa wa saratani,” amesema Prisclile.

Baadhi ya Wanawake wa Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakiwa kati_ika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Dk. Fredy Msemwa.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles