24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake Butiama kupewa mafunzo yakutumia Smartphone

Na Shomari Binda, Butiama

Shirika la Hope For Girls And Women in Tanzania lililopo Butiama mkoani Mara linatarajia kuendesha mafunzo kwa Wanawake namna ya kutumia simu janja (Smartphone) kutoa taarifa juu ya masuala ta ukatili.

Mkurugenzi wa Shirika la Hope For Girls in Tanzania, Robhi Samweli akizungumza na Waandishi wa Habari

Mafunzo hayo ya siku mbili yanatarajiwa kuanza Alhamis Juni 17, 2021 kwenye kituo cha Nyumba Salama huku Wanawake 59 kutoka vijiji vya wilaya ya Butiama wakitarajiwa kushiriki mafunzo hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo Juni 16, 2021 Mkurugenzi wa Shirika hilo, Rhobi Samweli, amesema wanatoa mafunzo hayo ikiwa ni kufanikisha kupata taarifa.

Amesema licha ya mafunzo hayo watapewa pia simu janja kila mmoja zitakazowawezesha kutoa taarifa hizo za ukatili kwenye maeneo hayo.

Rhobi amesema kupitia program hiyo ambayo wanatoa mafunzo kwa kushirikiana na shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) kutoa simu janja 210 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 300 ili kuwawezesha wanawake.

“Taarifa ni kitu muhimu na tunashukuru Shirika UNFPA kwa kutoa simu janja kwa Wanawake kwa ajili ya kutoa taarifa juu ya masuala mbalimbali ya ukatili.

“Naamini baada ya mafunzo haya utoaji wa taarifa utakuwa mzuri na kusaidia kupambana na matukio ya ukatili,” amesema Rhobi.

Amesema mafunzo kama hayo tayari yalishatolewa wilayani Serengeti na kupata mafanikio katika utoaji wa taarifa za matukio ya ukatili ksenyr maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles