28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto Mara wapaza Sauti kupinga ukatili

Na Shomari Binda, Butiama

Watoto mkoani Mara wamepaza sauti na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali wazazi wanaowafanyia ukatili majumbani.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 16, 2021 na Watoto wanaolelewa kwenye kituo cha nyumba Salama kulichopo Butiama mkoani Mara baada ya kutembelea na Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilayani humo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika.

Wamesema wapo wazazi ambao wamekuwa chanzo cha kunyanyaswa kwa watoto na kushindwa kutimiza ndoto zao zikiwemo za kielimu.

Mmoja wa Watoto hao aliyejitambulisha kwa jina la Maria Robert, mkazi wa Tarime amesema amepitia wakati mgumu katika malezi yake kabla ya kusaidiwa na kituo cha nyumba salama.

“Baba yangu alikuwa hataki nisome na kutaka nikeketwe lakini Mama alinisaidia kunihamisha nyumbani na kuendelea na masomo.

“Lakini bado baba alinifatilia na kutaka niache masomo na kusamua kuja nyumba salama ili kupata msaada nashukuru leo niko hapa na kuiomba serikali kuwasaidia watoto,” amesema Maria.

Mwenyekiti wa (UWT) wilayani Butiama, Anna Josephat, amesema Wanawake wanapaswa kuwa mabalozi wa kupinga masuala ya ukatili kwa watoto.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Nyumba Salama, Rejina Lucas amesema kwenye kituo hicho wamekuwa wakitoa elimu ya ujasriamali ili kuweza kuwasaidia.

Amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwapa malezi bora watoto ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ili kuweza kufikia ndoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles