25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume wafanyiwa ukatili na wake zao

Hadija Omary -Mtwara

WAKATI dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake Machi 8 ya kila mwaka kwa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, hali imekuwa tofauti wilayani Tandahimba mkoani Mtwara  ambako vinara wa kufanyiwa ukatili wamekuwa ni wanaume.

Hayo yalisemwa juzi mjini hapa na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Tandahimba, Francis Mkuti kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Sebastian Waryoba wakati wa sherehe za Siku ya Wanawake katika Kijiji cha Chingungwe wilayani humo.

Mkuti alisema kuwa licha ya mashirika na asasi mbalimbali za kiraia na zisizo za kiserikali za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, lakini bado kina mama wa wilaya hiyo wamekuwa vinara wa kuwafanyia ukatili waume zao.

“Kuna kinamama wanawafanyia ukatili waume zao, kuna kina mama wababe wanawapiga waume zao, ‘wanawapiga biti’, wakikaribia kupanda kitandani wanawaambia piga magoti hapo leo hupati mpaka useme ulikuwa wapi, mnatutaabisha sio vizuri,” alisema Mkuti.

Alisema kuwa pamoja na mateso na ukatili huo wanaofanyiwa wanaume, lakini bado wameonyesha kuwa wavumilivu na kubakia kukaa kimya kwa kuona aibu kueleza yanayowakuta.

Kwa upande wake, Ofisa Mradi wa Kuboresha Huduma za Kisheria (LIWOPAC), Fatuma Nyama alisema kuwa  takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 77 ya mashauri mbalimbali yanayopokewa kwa wasaidizi wa kisheria, yanahusiana na wanawake huku asilimia 23 yakiwa ni ya wanaume.

Alisema kuwa kati ya mashauri 558 yaliyopokewa shirika hilo kwa mwaka jana, mashauri 430 yaliripotiwa na wanawake na 128 wanaume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles