25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Wafuasi Chadema wafurika Mahakamani hukumu ya kina Mbowe

KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imefurika wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ulinzi umeimarishwa kwa askari kila kona saa tatu kabla ya muda wa hukumu ambapo kati ya waliohudhuria ni mwanachama wa chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif .

Wafuasi hao walianza kumiminika eneo la mahakama tangu saa moja asubuhi wakisubiri hukumu ya vigogo wa Chadema akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe inayotarajiwa kusomwa saa nne na nusu asubuhi hii.

Hukumu hiyo inasomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba , mahakama inafikia hatua hiyo baada ya miaka miwili ya kesi hiyo kufika katika Mahakama ya Kisutu na mwaka mmoja kasoro siku nne kwa Hakimu Simba kupokea jalada na kuanza kusikiliza upya kesi hadi kufikia mwisho.

Awali kesi hiyo ilipoanza Machi mwaka juzi ilikuwa inasikilizwa na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye aliyeuliwa kuwa Jaji Machi mwaka 2019 na jalada la kesi hiyo kuhamia kwa Hakimu Simba Machi 14 mwaka 2019.

Kina Mbowe washtakiwa kwamba Februari 16 mwaka 2018 maeneo ya Uwanja wa Buibui katika Kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni, walifanya maandamano, walitoa maneno ya uchochezi yenye lango la kuwashawishi wananchi kuichukia Serikali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles