20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

WANASHERIA WAMWEKA MATATANI MKE WA MUGABE

HARARE, ZIMBABWE


WANASHERIA wamemfungulia kesi Grace Mugabe, mke wa Rais wa zamani, Robert Mugabe, wakimdai Dola za Marekani 278,000 (Sh milioni 635 za Tanzania).

Hatua hiyo inakuja ndani ya wiki mbili tangu Mugabe atangaze hadharani kwamba asigekipigia kura chama chake cha Zanu-PF wala mgombea urais na mrithi wake, Emmerson Mnangagwa.

Badala yake katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 30, alimpigia kura kiongozi wa muungano wa upinzani wa MDC Alliance, Nelson Chamisa.

Hata hivyo, mgombea huyo hakushinda na wafuasi wake walimlaumu Mugabe kwamba alichangia kushindwa kwa Chamisa na sasa Grace amejikuta kwenye matatizo mengine.

Mwanamama huyo aliyetamba enzi zake, alidai kupoteza Dola za Marekani milioni 1.2 baada ya kutaka kununua pete ya almasi kwa maadhimisho ya ndoa yake.

Wakati huo aliwaajiri wanasheria kutoka kampuni ya uanasheria ya Manase ili wamsaidie kupata fedha zake, alizodai alidhulumiwa na mfanyabiashara wa almasi kutoka Lebanon, Jamal Ahmed.

Wanasheria hao sasa wamemgeuzia kibao wakisema Grace na mtoto wake Russell Goreraza, walishindwa kuwalipa ujira katika kesi hiyo waliyomsimamia na nyingine kadhaa.

Kwa mujibu wa hati za madai kutoka Mahakama Kuu, wanasheria hao wanataka walipwe dola 278 304.05 kama gharama za kisheria sambamba na asilimia 10 ya riba kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles