29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, October 2, 2022

VATICAN YALIFUNGIA SHIRIKA LA WATAWA

KAMPALA, UGANDAMAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki duniani, Vatican, yameamuru kusitishwa kwa shughuli za Shirika la Watawa wa Mitume wa Yesu na kuliweka chini ya Tume ya Uchunguzi ya Kipapa.

Hatua hiyo kali iliamriwa na Kardinali Joao Braz de Aviz, anayesimamia mashirika ya shughuli na maisha ya kitawa, ambaye pia alimteua Mchungaji Fr. Raphael p’Omony Wokrach wa Taasisi ya Misheni ya Kitawa ya Camboni (MCCJ) kuongoza tume hiyo.

Tume hiyo imepewa jukumu la kusimamia na kupitia shughuli za uongozi wa shirika na kuendesha uchunguzi juu ya nyendo mbovu za mapadri.

“Amri hii inazuia kuingizwa kwa wanachama wapya shirikani na kuendeleza taaluma za kidini na kusimamishwa kwa upadirisho wa mapadre,” alitangaza Kardinali de Aviz.

Fr. Wokrach aliongoza uchunguzi wa awali, ambao umesababisha kusitishwa kwa shughuli za shirika hilo, ambalo lilitiwa hatiani kwa kile Vatican ilichokiita ‘matatizo makubwa na mapungufu ya kutisha kuhusu misingi na maadili ya kidini, uchaguzi wa wagombea na wanachama, staili ya maisha na utume’.

Mbali ya kusitisha shughuli za upadirisho, Vatican pia ilitangaza kufungwa kwa seminari za shirika hilo zenye makao makuu Nairobi, Kenya na kuagiza kupitiwa kwa mfumo wa kiuchumi na kifedha, unaowasaidia wanachama kuishi maisha kwa mujibu wa kiapo cha umasikini kulingana na katiba.

“Tume itathibitisha kesi za wanachama wanaoishi kinyume na kiapo chao, kufuatia maagizo ya kusanyo la Injili ya watu, kwa makubaliano na Askofu Mkuu wa Nairobi,” alitangaza Kardinali De Avidz.

Shirika hilo ni la kwanza la kitawa kuanzishwa barani Afrika Agosti 22, 1968 likianzia nchini Uganda kabla ya kuenea Kenya, Tanzania, Sudan na kwingineko Afrika, Ulaya, Australia na Marekani.

Mwaka 2008, shirika hilo liliadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa na lilipanga kuadhimisha miaka 50 baadaye mwezi huu.

TEC YANENA

Akizungumzia uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Dk. Charles Kitima, aliliambia MTANZANIA jana kwa simu kuwa suala la kusimamisha shirika la utawa nchini Uganda halihusiani na Tanzania, hivyo hawezi kulizungumzia.

Alisema kama angesimamisha Papa Mtakatifu Francis, wangepewa na Tanzania, lakini suala la shirika hilo hawawezi kupewa taarifa yoyote.

“Kila nchi ina taratibu zake na sisi mambo ya mtandao hatuwezi kushughulikia, ni vema mkawatafuta Waganda wenyewe waweze kuzungumzia suala hilo, wao ndio wanaolijua na si hapa Tanzania.

“Na hata mkienda kwenye Shirika la Mitume kwa hapa Tanzania, hawawezi kusema lolote kwa sababu wao si wahusika,” alisema Dk. Kitima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,474FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles