29 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Wanasheria wamkimbia Jacob Zuma

Johannesburg, Afrika Kusini

Huku kesi ya rushwa inayomkabili Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ikitarajiwa kusikilizwa mwezi ujao, mwanasiasa huyo amepata pigo la kukimbiwa na wanasheria wake.

Taarifa mpya ni kwamba wanasheria wake wamejiweka kando kumsimamia Zuma kwa kuwasilisha ombi lao mbele ya Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg.

Mmoja ya wanasheria hao ni Eric Mabuza lakini hakuweka wazi sababu iliyomfanya kufikia uamuzi huo wa kumpa kisogo bosi wake huyo.

Zuma, mwenye umri wa miaka 78, anashutumiwa kuwa alipokea rushwa kutoka kwa kampuni ya elektroniki na ulinzi Thales katika mkataba wa silaha wenye thamani ya Rand milioni 4, karibu euro 216,000 kwa bei ya sasa, uliyotolewa mwaka 1999.

Jacob Zuma na kampuni ya Thales wameendelea kukanusha tuhuma hizo.

Mpango wa silaha ulifanyika mwaka 1999 mwaka ambao bwana Zuma alihama kutoka mkuu wa jimbo kuwa makamu wa rais. Anashtakiwa kwa kukubali kuchukua malipo yasiyokuwa halali 783

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles