22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Biden afurahia polisi kukutwa na hatia

Washington, Marekani

Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema kukutwa na hatia kwa ofisa wa polisi aliyemuua George Floyd ni ushindi, ingawa zinahitajika juhudi zaidi kutokomeza ubaguzi.

Polisi wa kizungu, Derek Chauvin, alinaswa na kamera za CCTV akiwa amemwekea goti la shingo Mmarekani mwenye asili ya Afrika, Floyd, adhabu iliyosababisha kijana huyo apoteze maisha.Baada ya maandamano ya haoa na pale kulaani tukio hilo, jana Chauvin alikutwa na hatia na huenda sasa ofisa huyo akakumbana na adhabu ya kifungo cha gerezani.

Majaji nchini Marekani wamempata na hatia afisa wa polisi wa zamani kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd huko Minneapolis mwaka jana.

Derek Chauvin (45), alinaswa katika kanda ya video akipiga goti kwenye Shingo ya Floyd kwa zaidi ya dakika tisa alipokamatwa mwezi Mei, mwaka uliopita.

Video hiyo iliyotazamwa sana iliibua hisia kali na kusababisha maaandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi kote duniani na utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaofanywa na kikosi cha polisi.

Chauvin alipatikana na makosa matatu: mauaji ya kiwango cha pili, kiwango cha tatu na mauaji bila kukusudia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles