Meya ataka shule ya King’ongo kupewa jina la Magufuli

0
261

Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jafari Juma, amependekeza Shule ya Msingi iliyopo Kimara King’ongo kuitwa jina la hayati Dk. John Magufuli.

Akizungumza na Mtanzania Digital mapema leo Aprili 21, 2021 jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Elirehema Kaaya ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo manispaa hiyo, Meya amependekeza jina la Magufuli kwa kuwa aliipenda na ndio chanzo cha maendeleo ya shule hiyo.

“Ikiwa ni sehemu ya kumuenzi hayati Magufuli kwa kuwa alitamani kuja kutembelea na kuangalia maendeleo ya shule hii, tunapendekeza kuitwa jina lake kutokana na kuipenda na kutaka kuja kuiona lakini hakuweza kujakuiona” amesema Meya Juma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here