29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi 700 Lindi walipwa fidia kupisha mradi madini ya bunyu

Hadija Omary, Lindi

Wananchi 776 wa vijiji saba wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wamelipwa fidia ya zaidi ya Sh bilioni 7.45 ili kupisha mradi wa uchimbaji madini ya bunyu (Graphite).

Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Kampuni ya Urenix Tanzania, Alley Mwakibole akizungumza na Mtanzania Digital leo Alhamisi Januari 17, mjini hapa.

“Mradi wa uchimbaji na utengenezaji bidhaa zinazotokana na madini ya bunyu utaanza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ulipaji fidia ya ardhi ya kilomita za mraba 30 na mazao kwa wananchi wa vijiji vya Matambarale Kusini, Matambarale Kaskazini, Chiundu, Chunyu, Mihewe, Namkatila na Namikulo.

“Watu 776 waliopisha mradi kati 785 wamelipwa fidia ya Sh bilioni 7.258 na milioni 48.800 zimelipwa kwa ajili ya maeneo ya kimila na kidini huku watu 59 wanatarajiwa kujengewa nyumba za makazi ambazo zitagharimu kiasi cha Sh bilioni 3.45.

Hata hivyo, Mwakibole amesema watu tisa kati yao hawajalipwa fedha zao kiasi cha Sh milioni 147.906 baada ya wananchi hao kugomea fidia kwa madai kuwa ni ndogo hazilingani na maeneo yaliyochukuliwa. 

Hata hivyo katika kikao chake na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa Lindi, Godfrey Zambi, amesema kutokana na kampuni hiyo kutimiza masharti yote,  mkoa umeridhia kuanza kutekelezwa kwa mradi huo.

“Serikali inatambua umuhimu wa mradi huo kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na nchi kwa ujumla, wananchi mnatakiwa kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo pindi mradi utakapoanza kutekelezwa pamoja na kuchangamkia fursa ya mradi huo kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi,” amesema Zambi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles