24.6 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi 342 Misenyi walilia fidia

Na Mwandishi Wetu, Misenyi

WANAKIJIJI 342 wa vijiji vya Bulembo, Mushasha na Bugolola waliofanyiwa tathimini  kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Ndege wa Kimataifa wa Omukajunguti wilayani Misenyi mkoani Kagera, wamesema wanakerwa na udanganyifu mkubwa unaofanywa na Serikali juu ya malipo ya fidia kwa miaka sita sasa.

Wanakijiji hao walikutana juzi katika ofisi ya Kata ya Mushisha  ili kujadili hatima yao ambapo kwa kauli moja, waliamua kuunda kamati ya watu 16 ili kufuatilia fidia ya malipo yao.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu wa Kamati hiyo, George Sebastian alisema tangu wananchi hao wafanyiwe tathimini mwaka 2010, walizuiliwa wasifanye au kuendeleza shughuli zozote za uzalishaji katika maeneo yao.

“Tangu mwaka 2010, wananchi wameuzuliwa kufanya shughuli za uzalishaji katika maeneo yao, mpaka sasa hakuna fedha za fidia zilizolipwa.

“Mwezi huu tumepokea barua inayowataka wananchi walipwe ili waondoke kwenye mashamba yao…lakini ukweli hakuna lolote lililofanyika,”alisema Sebastian.

Alisema Novemba mwaka huu, alipokea barua kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliyomtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ndege Tanzania kuwalipa fidia wananchi hao pamoja liba kutoka benki husika tangu Julai, mwaka huu kwani muda waliostahili kulipwa, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika.

Alisema nakala ya barua hiyo, imetumwa ofisi zote za  Serikali wilayani Misenyi.

“Kama tunavyojua hakuna mwananchi anayejua atalipwa kiasi gani kwa kuwa hatutakutajia ardhi, mimea au majengo yanathamani gani.

“Kamati iliyoundwa inatakiwa kwenda kwa mkurugenzi Jumatatu (leo) ili aipatie orodha ya majina ya wananchi wanaostahili kulipwa fidia…ikishindikana tutaamua nini cha kufanya,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Wananchi hao walidai kuwa tathimini hiyo ilikuwa ni danganya toto kwa sababu kila mmoja alikuwa anajifanyia tathimini yake mwenyewe na kuja na taarifa kwenye fomu za wajumbe waliokuwa wametumwa na Serikali.

Mmoja wa wananchi hao, Wilfred Bwajala alisema kauli zinazotolewa na Serikali juu  ya ujenzi wa uwanja huo zimerudisha nyuma maendeleo yao kutokana na kuzuiwa kufanya shughuli za maendeleo karibu miaka sita sasa.

Alisema kama watakosa majibu ya msingi, watachangishana fedha kwa ajili ya kwenda ngazi za juu, hasa kuona na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa.

“Tukikosa majibu ya kuridhisha kutoka kwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi, tupo tayari kwenda ngazi za juu…hatuwezi kuona haki yetu inapotea hivi hivi,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles