23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wanajeshi wa Poland kutegua bomu hatari

WARSAW, POLAND

WAPIGA mbizi wa jeshi la Poland wameanza operesheni ya hatari ya kunasua bomu kubwa la Uingereza lililotumika kwenye vita vya pili vya dunia lililo chini ya bahari.

Karibu wakazi 750 wameondolewa kutoka kwenye eneo hilo karibu na mji wa bandari wa Swinoujscie na operesheni hiyo inatarajiwa kuchukua siku 5.

Bomu liitwalo Tallboy, au bomu la ”tetemeko la ardhi” lina urefu wa mita 6 na uzito wa tani 5.4.

Bomu hilo lilidondoshwa wakati wa uvamizi mwaka 1945 ambapo tukio hilo lilizamisha meli ya Ujerumani ya Lützow.

Bomu hilo liko chini umbali wa mita 12 na kinachoonekana juu kikichungulia ni sehemu ya pua ya kifaa hicho.

Mabomu ya Tallboy yalidondoshwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia

Kazi iliyopo sasa ni kuhakikisha bomu hilo linaondolewa kwa kutumia combo maalumu kutoka mbali, na wapiga mbizi tayari wameliandaa eneo hilo kwa siku kadhaa.

Bomu hilo liligundulika wakati wa kufanya usafi wa bahari mwaka jana.

Poland haijawahi kunasua bomu kubwa kama hilo chini ya maji hapo kabla. The Tallboy ni bomu linalosababisha mtetemeko ,linalopenya chini, lililoundwa kwa ajili ya kuangushwa karibu na eneo linalolengwa na kufanya uharibifu kwa kulipuka na kusababisha tetemeko na mshtuko mkubwa.

Majeshi ya anga ya Uingereza yaliangusha mabomu ya aina hiyo mwaka 1944-45 kwa kutumia ‘Lancaster bombers’ na maeneo ya kurushia roketi ya jeshi la Ujerumani Nazi – V yalikua miongoni mwa maeneo yaliyokuwa yakilengwa.

Poland ni moja kati ya nchi zilizoath vibaya kwenye vita hivyo-mji mkuu Warsaw uliharibiwa vibaya na wajerumani.

Poland bado inahesabu athari kutokana na vita vya pili vya dunia.

Mlipuko unaodhibitiwa unaelezwa kuwa hatari sana kwa sababu utasababisha mlipuko mkubwa sana ambao utaharibu mali za watu walio mbali na eneo hilo,Mwandishi wa habari wa BBC Adam Easton anaripoti kutoka mjini Warsaw .

Baadhi ya wakazi wamekataa kwenda kwenye makazi ya muda mfupi kwenye jengo la michezo kwa hofu ya kuambukizwa virusi vya corona.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles