20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Sudan yaonywa kuhusu machafuko

KHARTOUM, SUDAN

MKUU wa zamani wa Baraza la Fiqhi ya Kiislamu la Sudan ameonya kuwa machafuko yatatokea nchini humo endapo wananchi watalazimishwa kukubali nchi yao ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Abdurahim Ali ameashiria upinzani wa vyama vingi vya siasa, asasi na shakhsia wanaoheshimika nchini Sudan dhidi ya hatua ya kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na akasisitiza kuwa, kuanza hatua za utekelezaji kwa lengo la kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo haramu kutakabiliwa na upinzani kamili wa wananchi wa Sudan.

Abdurahim Ali aliongeza kuwa, kwa wastani, zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Sudan wanapinga nchi yao kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Mkuu wa zamani wa Baraza la Fiqhi ya Kislamu la Sudan amesisitiza kuwa, kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kunamaanisha kuvamiwa na kukaliwa ardhi nyingine zaidi za Wapalestina na kuzidi kupotea haki za wananchi hao madhulumu.

Imarati imekuwa nchi ya kwanza katika miaka ya karibuni kuanzisha uhusiano na Israel

Baada ya Imarati na Bahrain kutangaza uamuzi wa kiuhaini na usaliti wa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni, tarehe 15 Septemba, nchi hizo mbili ndogo za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi zilisaini rasmi mikataba ya kuanzisha uhusiano huo wa kidiplomasia na kuutambua rasmi utawala bandia wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House na kuhudhuriwa na rais wa Marekani Donald Trump na waziri mkuu wa utawala huo wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.

Hatua hiyo ya Imarati na Bahrain imelaaniwa na kukabiliwa na upinzani mkubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles