32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wanahabari watakiwa kuelimisha jamii kuhusu TB

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wito umetolewa kwa Waandishi wa Habari nchini kutoa Elimu iliyo Sahihi juu ya ugonjwa wa Kifua kikuu kwa jamii ili kuepusha kuwepo na habari zinazoleta mkanganyiko kwa watu wenye dalili za ugonjwa huo.

Wito huo umetolewa Machi 14, 2023 na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Reginald Mlay alipokuwa akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mganga Mkuu wa Jiji .

“Tunategemea mchango wenu usiishie tu katika kuripoti bali uendelee na tunategemea siku hiyo Waziri Mkuu aseme kuwa Vyombo vya habari vimefanya kazi nzuri, Tulipoti habari za kweli na za uhakika kutokana na kile tunachoelekezana hapa,” Dk. Mlay.

Amesema mpango huu wa Mapambano ya Kifua Kikuu ilianzishwa 2018 ambapo kwa Tanzania ulianza 2021 ukiwa na kazi ya kuwaleta wadau pamoja.

Hivyo, mwaka huu tunalenga mafunzo haya kwa Wanahabari kuwa na tija zaidi ndiyo sababu tumekusanya kada zote.

Dk. Mlay alitoa wito kwa Wanahabari nakusema: “Niwaombee tushiriki kikamilifu peke tuweze kwenye lengo letu na tulifikishe panapotakiwa Sasa hivi Kuna taharifa kwenye Maeneo tofauti na zinaifikia jamii lakini zinaweza zisiwe sahii na wakipata taarifa sahii watashirikiana na sisi,” amesema Dk. Mlay.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,400FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles