33.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

LHRC, Sheikh Ponda waomba Serikali kuwaachia huru Masheikh waliko gerezani

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kwa kushirikiana na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda kimetoa wito wa kuachiwa huru au kutendewa haki ya kujitetea Mahakamani Masheikh wakiwemo familia ya marehemu Sheikh Said Mohammed.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo mapema Machi 15, 2023 katika Ofisi za Makao Makuu ya LHRC jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Anna Henga amesema Sheikh Said Mohammed alifariki duani Machi 4, 2023 akiwa mahabusu katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

“Marehemu Sheikh Said Mohammed alikuwa akituhumiwa kwa kuhuma za Ugaidi ambapo aliwekwa katika Gereza la Segerea na hatimaye Ukonga tangu mwaka 2016, ikiwa ni miaka 7 sasa mpaka umauti ulipomfika,” amesema Henga.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishina wa magereza Afande Ramadhani Nyamka machi 9, 2023, marehemu Sheikh Said Mohammed alifariki kwa tatizo la shirikizo la damu.

Pia Henga aliagiza ufanyike uchunguzi wa kina juu ya nini hasa chanzo cha kifo cha marehemu Sheikh Said Mohamed na utaratibu huo uendelee kwa watu wote wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola

Kadhalika, Henga iwaachilie huru au iwape haki ya kujitetea mahakamani watuhumiwa wote waliokaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja bila ya mashauri yao kusikilizwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,079FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles