23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI 261 WATIWA MIMBA TANGA

Na OSCAR ASSENGA-TANGA


WANAFUNZI 261 wa shule za msingi na sekondari Mkoa wa Tanga, wametiwa mimba kuanzia Januari 2015 hadi Oktoba 2016.

Takwimu hizo zilitolewa jana na Ofisa Elimu Taaluma Mkoa wa Tanga, William Mapunda, alipokuwa akizungumza kwenye Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga.

Kwa mujibu wa Mapunda, miongoni mwa wanafunzi hao, 55 ni wa shule za msingi na 206 ni wa shule za sekondari.

“Hali hiyo imechangiwa kwa asilimia kubwa na kuwapo kwa ngoma za usiku maarufu kama baikoko na vibanda vinavyoonyesha picha za video.

“Kimsingi, naweza kusema tatizo la mimba za utotoni limekuwa kubwa na tunafanya kila tunaloweza ili kulikomesha,” alisema Mapunda.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella, aliwaagiza

wakuu wa wilaya kuhakikisha wanasimamia tatizo hilo kwenye shule za msingi na sekondari kwa  kuwafikisha kwenye vyombo vya

sheria wanafunzi wanaopata ujauzito ili wawataje wahusika kwa ajili ya kuwachukulia hatua.

“Hatuwezi kupiga hatua za kimaendeleo

kwenye sekta ya elimu kama suala hili halitapatiwa ufumbuzi. Kwa hiyo, ni muhimu wahusika wachukuliwe hatua za haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini Mkoani Tanga, Asseli Shewally, alitaka kuwapo na ushirikiano baina ya wazazi, walimu

na viongozi ili kumaliza tatizo hilo.

Pia, alitaka iwepo mikakati itakayosaidia kukomesha vitendo hivyo kwa kuwashtaki watakaobainika kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

“Lazima iwepo mikakati maalumu itakayowanasa wahusika wote kwani bila kufanya hivyo, watu hao watazidi kuwatia mimba watoto wetu na kuwaharibia maisha,” alisema Shewally.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles