27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Wamachinga Dar wataka bei elekezi vifaa tiba vya corona

Christopher Gauluhanga Na Sabina Wandiba -Dar es salaam

UMOJA wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam (Kawasso), wameiomba Serikali itoe bei elekezi au utaratibu maalumu huhusu upatikanaji wa vifaa tiba, kinga na dawa za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona Covid 19.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi katika mahojiano maalumu jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kawasso, Namoto Namoto amesema hivi sasa kumeibuka uuzaji holela wa bidhaa zinazotumika kutokomeza maradhi hayo jambo ambalo linafaya wananchi wengi washindwe kumudu.

Alisema upandaji holela wa vifaa hivyo unaweza kuchangia kuzidi kukithiri kwa maambukizi ya ugonjwa huo hapa nchini.

“Wakati sasa umefika kwa Serikali kuamua kutoa bei elekezi au kushusha bei ya vifaa vinavyotumika na dawa kuzuia ugonjwa wa corona kwa kuwa wafanyabiashara wametumia ugonjwa huo kama fursa ya kujinufaisha na kupandisha bei kwa kasi kila kukicha,”alisema Namoto.

Akitolea mfano wa bidhaa ya maski ambayo hutumika kuzuia maambukizi, awali ilikuwa inauzwa Sh 5,000 kwa boksi lakin hivi sasa imepanda na kufikia Sh 45,000 hadi Sh 50,000.

Alisema ni vema Serikali ikaamua kuhamasisha wananchi wapunguze gharama za vifaa hivyo na dawa kwa sababu hilo ni janga lankitaifa na kidunia.

ATHARI ZA UGONJWA

Alisema asilimia 20 ya bidhaa zinazouzwa madukani hapa nchini zinatokea China hivyo kwa sasa zimepungua uingiaji kwa sababu ya maambukizi.

Alisema tangu kuanza kwa maambukizi hayo idadi ya wateja wanaofika kununua bidhaa imepungua tofauti na siku za nyuma kwa sababu wengi wanahofia msongamano.

Alisema kama wamachinga wamejipanga kujiimarisha kibiashara, lakini wameanza kukabiliwa na uhaba wa bidhaa kwa sababu ya kuibuka kwa  ugonjwa huo.

Akizungumzia kuhusu mikopo alisema zaidi ya wafanyabiashara 360 wamenuifaka na mikopo  ikiwamo wa Jiwezeshe ambayo unatolewa na Kawasso na Benki ya Biashara CRDB.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles