23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

DC Singida aanzisha mfuko kudhibiti corona

Nathaniel Limu -Singida

MKUU wa Wilaya ya Singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) na wadau mbalimbali wa mkoa wa Singida, Pascas Mrangila, ametoa wito kwa wadau ndani na nje ya mkoa kuchangia mfuko wa kudhibiti ugonjwa hatari wa corona.

Alitoa wito huo juzi muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha kamati ya PHC.

Alisema kamati ya afya ya msingi na wadau wake, wamepanga bajeti za kukusanya Sh milioni 556 fedha ambazo zitatumika kugharamia mapambano 

“Tumepanga bajeti hiyo, lakini hadi sasa hatuna fedha kwa ajili ya mapambano hayo. Tuna imani wadau wa ndani na nje ya mkoa watajitokeza mapema kuchangia mfuko huu.

“Sote tukishikamana vizuri tukapata nguvu ya fedha tunazozitarajia, tukazingatia maagizo na maelekezo na Mungu akatutangulia, mkoa wetu utakuwa salama,”alisema.

Akisisitiza, mwenyekiti huyo alisisitiza kwamba mkoa kwa ujumla umejipanga kikamilifu kukabiliana na virusi vya corona, ili visilete madhara.

Aidha, alitoa wito kwa wamiliki wa nyumba za kulala wageni, wahakikishe wanatoa taarifa sahihi za wageni wakiwemo wa kutoka nje ya mkoa.

“Kwa sasa msimu wa kuuza vitunguu mkoani hapa umepamba moto, kuna wafanyabiashara kutoka mikoa mingine na nje ya Tanzania. Wageni hawa ni lazima taarifa zao zijulikane mapema. Kila mkazi wa mkoa wa Singida, ajitume kupambana  na ugonjwa huu wa Corona”,alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles