28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Walimu matatani kwa tuhuma zakutapeli wenzao wastaafu Sh milioni 45

Gurian Adolf – Sumbawanga

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Rukwa, inawashikilia viongozi wanne wa Ushirika wa Walimu wa Akiba na Mikopo (UWAMI – Saccos (Ltd)) kwa kuwatapeli walimu wastaafu amana zao zenye thamani ya Sh milioni 45.5.

Inadaiwa walimu wastaafu ambao ni wanachama wa UWAMI- Saccos wamekuwa wakidai kulipwa amana zao kwa zaidi ya miaka mitano huku wadai wengine watatu wakiwa wamefariki dunia bila kulipwa stahiki zao.

Baada ya kuswekwa rumande kwa siku nne, watuhumiwa hao walikubali kuwalipa walimu 13 wastaafu Sh 11,541,750/  ikiwa ni amana yao waliokuwa wakiiidai Saccos hiyo kwa miaka mitano iliyopita.

Wanachama wa UWAMI – Saccos ambayo iliyoanzishwa rasmi 2004 iko katika manispaa ya Sumbawanga huku wanachama wake wakiwa ni walimu wa shule za msingi na sekondari.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda, aliwataja viongozi hao ambao pia ni walimu kuwa ni  Marietha Haule ambaye ni Mwenyekiti wa UWAMI – Saccos iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga.

Wengine ni Alexander Zumba, Anicet Lyela na Benard Msika huku mwingine wa tano ambaye majina yake hakuyataja anadai wamekimbia na kujificha kusikojulikana.

Mwenda akimkabidhi fedha hizo mwenyekiti wa kundi la walimu 13 wastaafu Grayson Mwasumbi, aliwapatia mwezi mmoja watuhumiwa hao wawe wamekabidhi taasisi hiyo Sh milioni 34 wanazodaiwa na walimu wastaafu

“Hawa walimu wastaafu 13 walifika ofisi kwetu wakilalamika kuwa watuhumiwa wamekataa kuwalipa amana zao baada ya kustaafu miaka mitano iliyopita.

“Walilalamika kuwa watuhumiwa walikuwa wakitumia lugha ghadhibishi iliyojaa maneno ya shombo huku wakiwatishia waendeshe kushtaki popote lakini kamwe hawatalipwa amana zao, hivyo walifika ofisini kwetu ” alieleza

Aliongeza maofisa wa taasisi hiyo waliwasaka na kuwakamata watuhumiwa wanne kati ya watano ambapo baada ya mahojiano waliwekwa rumande .

 “Waliwekwa rumande kuanzia Jumatatu hadi Jumatano baada ya hapo walikubali kuuwalipa walimu wastaafu 13 Sh 11,541,750  ambazo walizikabidhi kwa Takukuru na leo  tunawakabidhi fedha hizi ,” alieleza.

Akizungumza na gazeti hili Mwenda amethibitisha kuwa watuhumiwa wote wanne wamekamatwa tena kwa mahojiano na maofisa wa taasisi hiyo baada ya kubaini  madudu mengi waliyoyafanya.

Mwenyekiti wa muda wa kundi la walimu wastaafu 13, Mwasumbi aliishukuru taasisi hiyo kwa kuwarejeshea fedha ambazo waliamin .kuwa wametapeliwa

Huku mmoja wa mwalimu mstaafu Mary Chale alisema wameteseka kwa miaka mingi wakifuatilia kulipwa amana amana zao hadi soli za viatu vyao kutibika.

Naye mstaafu mwingine, Edward Mwambene alisema kinachosikitisha wenzao watatu wamekufa bila kulipwa amana zao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles