25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Adaiwa kumkata mumewe korodani baada Ya kunyimwa Sh 10,000 ya matumizi

SAM BAHARI – SHINYANGA

MKAZI wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, Shaibu Jabuka (36) anadaiwa kujeruhiwa kwa kukatwa korodani kwa wembe na mke wake aliyefahamika kwa jina moja la Mwajuma, baada ya kumnyima Sh 10,000 ya matumizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Deborah  Magiligimba, alisema tukio hilo lilitokea Aprili 6 mwaka huu, saa 7.00 usiku huko Ngokolo nyumbani kwa wanandoa hao.

Kamanda Magiligimba alisema Chanzo cha tukio hilo ni Mwajuma kunyimwa na mumewe Sh 10,000 ya matumizi.

Alisema siku ya tukio majira ya saa saba usiku wakiwa wamelala nyumbani kwao, Jabuka alianza kuomba  tendo  la ndoa kwa mkewe ambaye naye alianza kuomba apewe fedha za matumizi kwanza ndipo washirika tendo hilo.

Kamanda  Magiligimba  alisema katika mabishano hayo mwanaume huyo alianza kutumia nguvu kwa kumgeuza mkewe akihitaji kufanya tendo hilo.

Inadaiwa baada ya mwanaume kufanikiwa kufanya tendo la ndoa na mkewe, mwanaume alilala na ndipo mke wake alipoamka na kumkata mumewe korodani ya kulia kwa kutumia wembe.

Alisema  Jabuka alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa na kurejea nyumbani kwake.

Alisema Mwajuma  alitoroka  mara baada ya tukio na kukimbilia kusikojulikana na kwamba juhudi za kumtafuta  zinaendelea na atakapokamatwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda  Magiligimba alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga hususani wanandoa au wenye mahusiano ya kimapenzi, kuacha oja kujichukulia sheria mkononi bali wafikishe migogo yao kwa  wazee wenye busara, Ofisi za Ustawi wa Jamii na Dawati la Jinsia na Watoto zilizoko katika vituo vya polisi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles