29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 11, 2024

Contact us: [email protected]

WAKULIMA WATISHIA KUACHA KULIMA TUMBAKU

WAKULIMA wa tumbaku mkoani Katavi, wametishia  kuacha kulima zao hilo kutokana na kutolipwa fedha zao za mauzo ya msimu huu wa tumbaku.

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni za ununuzi wa zao hilo msimu huu kushindwa kununua tumbaku kutoka kwa wakulima kwa madai vyama vya msingi  vimezalisha ziada kubwa ya zao hilo .

Wakizungumza  na Mtanzania Digital, baadhi ya wakulima hao wamedai hawaoni sababu ya msingi ya kuendelea kuzalisha ziada ya zao hilo la biashara msimu ujao wa kilimo ambao unaanza Septemba kwa kuotesha mbegu kwa sababu hawajalipwa fedha zao za msimu uliopita huku tumbaku nyingine ikiwa imelundikana kwenye ghala na nyumba za wakulima.

“Tunadai fedha za msimu uliopita lakini pia tumbaku nyingine haijanunuliwa haijanunuliwa na Kampuni ya ununuzi  ya TLTC kwa kile kinachodaiwa uzalishaji  umezidi malengo waliyokubaliana baina ya Chama   cha Ushirika na Kampuni ya  TLTC, tumepoteza  kabisa matumaini ya kulima tena msimu ujao,” amesema mmoja wa wakulima hao.

Meneja wa Chama cha Msingi Mpanda Kati, Amani Rajabu amesema: “Kuhusu malipo ya mauzo yao ya tumbaku wakulima wenyewe waliamua  kwenye mkutano wao mkuu kuwa malipo yatakuwa yanafanyika baada ya masoko yote kuwa yamemalizika, hivyo kwenye chama hicho bado kuna kilo zaidi ya  500,000  hazijanunuliwa baada ya kuwa zimezidi kwenye makisio yao ya msimu wa kilimo wa  2016/2017.”

Msimu wa ununuzi wa zao hilo ulianza Mei    mwaka huu na ulisitishwa Septemba baada ya  kampuni  zinazonunua tumbaku kusitisha kununua baada ya idadi ya kilo walizokubaliana kimkataba na vyama vya ushirika kukamilika.

Mwisho

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles