24.5 C
Dar es Salaam
Monday, January 24, 2022

Wakulima wa pamba Shinyanga kuanza kulipwa fedha zao

MWANDISHI WETU

Mbunge wa Itima mkoani Shinyanga, Njalu Silanga (CCM), amewahakikishia wakulima wa pamba walipo katika jimbo lake kuanza kupokea fedha zao kuanzia sasa.

Silanga ameyasema hayo katika mkutano wake na wananchi uliofanyika katika Kijiji Cha Sunzula kata ya Mbita tarafa ya Kinamweli mkoani humo, uliolenga kutatua kero za wananchi na kutolewa kwa ufafanuzi wa mambo mbalimbali  na wakuu wa Idara.

Amesema anawahakikishia wananchi hao kuwa suala la pamba limeshamalizika na wakulima watalipwa fedha zao hivyo anawaomba waendelee kuwaamini.

“Rais alishazungumza kuwa akisikia mtu ananunua pamba chini ya Sh. 1,200 atapata shida kwahiyo Mwenyekiti nikwambie tu akikamatwa mtu wako anauza tofauti na maagizo wala usinipigie simu maana jambo hilo ni uhujumu uchumi.

“Serikali ipo macho na Rais anaona na kusikia kila kitu kinachofanyika katika maeneo yote ya nchi hivyo tuendelee kushirikiana naye na sisi hatutaki kuwanyonya wananchi tunataka kufanya kazi yenye faida,” amesema. 

Amesema Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, alipaswa kushiriki katika mkutano huo lakini ameshindwa kutokana na majukumu mbalimbali  ila anawahakikishia wakulima kuwa jambo hilo limekwisha na wakulima wote watalipwa fedha zao. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,326FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles