27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Nikki Mbishi awapa neno Jongwe, Profesa Jay

 GLORY MLAY

MSANII wa miondoko ya Hip Hop Bongo, Nikki Mbishi, amesema anatamani  kuona wakongwe wa muziki huo Profesa Jay na Sugu (Jongwe), wakianzisha kampuni za kusaidia tasnia na siyo kutoa nyimbo za kushindana na wasanii wapya.

Akizungumzia hilo, Nikki Mbishi alisema wasanii hao  ambao pia ni wabunge wa majimbo tofauti wana nafasi na uwezo mkubwa  wa kuwekeza kwenye tasnia.

“Sitarajii kuona wasanii hawa wanatoa ngoma na wanashindana kwenye chati na kina Country Boy au wasanii wengine, tunatamani kuwaona kama ma C.E.O,” alisema.

Nick Mbishi aliongeza kuwa huu ni muda wa Profesa Jay na Jongwe kushirikiana na wasanii kwa kuwa wana nafasi hoyo sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles