24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wakimbizi wa Kongo 200,000 wafukuzwa Angola

GENEVA, USWISI

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limesema raia wa Kongo 200,000 wengi wao wakiwa wakimbizi wamefukuzwa kutoka Angola kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Wakimbizi hao, ambao wengi wao walikuwa wanafanya kazi katika sekta ya madini wamerudi mwao wakiwa katika hali ya kukata tamaa.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Babar Baloch, raia wa Kongo wanalazimishwa kuvuka mpaka na kurudi kwao baada ya kufukuzwa kutoka Angola.

Uamuzi huo unatokana na hatua ya Serikali ya Angola ya kuwafukuza wahamiaji wa Kongo, ambao wengi wao walikuwa wakifanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya madini katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Angola.

Akizungumza na wanahabari mjini hapa juzi, msemaji huyo amesema shirika hilo lina wasiwasi juu ya ongezeko la hali itakayosababisha mgogoro wa kibinadamu katika Mkoa wa Kasai, ambako hali tayari ni tete.

Msemaji huyo ameleza pia juu ya msongamano wa watu katika mji wa Kamako uliopo Kasai, kwenye mpaka wa Angola.

Amesema hali hiyo imefikia kwa wau kulala nje, kwenye makazi ya familia nyingi zinazowakirimu, viwanja vya makanisa, na hata barabarani.

 

Katika baadhi ya maeneo ya Angola, kumekuwa na taarifa za mapigano na vurugu kati ya wahamiaji na mawakala wa utekelezaji wa zoezi hilo la kuwafukuza raia hao wa Kongo.

Maelfu waliofika mpakani, wametoa malalamiko yanayojumuisha unyanyasaji wa kijinsia, kupigwa na kusababishiwa majeraha ya mwili na wizi wa mali mikononi mwa vikosi vya usalama kutoka pande zote za mpaka.

Baloch amesema kufukuzwa kwa watu hao ni kinyume na mkataba wa Afrika juu ya haki za binadamu

Amesema UNHCR linaziomba Angola na Kongo kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha usalama na watu wanaovuka kutoka upande mmoja hadi mwingine kwa mpangilio maalum, pamoja na kuheshimu haki za binadamu na za wale walioathirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles