30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

WAKILI WA LEMA KUKATA RUFAA KUPINGA UAMUZI WA MAHAKAMA

Wakili Sheck Mfinanga anayemuwakilisha Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema, amewasilisha notisi ya mdomo ya nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha leo.

Mbele ya Hakimu Benard Nganga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mfinanga aliwasilisha notisi hiyo jana baada ya Hakimu kusoma uamuzi mdogo katika kesi ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano ya Septemba Mosi mwaka jana,inayomkabili Mbunge huyo. 

Sheck aliiomba mahakama mwenendo wa kesi hiyo pamoja na uamuzi huo kwa ajili ya rufaa hiyo na kuiomba mahakama kusitisha kuendelea na kesi hiyo.

Awali akisoma uamuzi huo Hakimu Nganga alisema baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote mbili mahakama imepitia hati ya mashitaka na kuwa suala la shauri kuwa na viashiria vya kikatiba ambavyo vinataka kesi hiyo kusikilizwa mahakama kuu mbele ya majaji watatu na kuwa mashahidi kushindwa kujibu maswali ya kikatiba yatakayojitokeza hivyo itasaidia upande wa utetezi.

Alisema kuwa suala la kikatiba kujitokeza kwenye kesi ni hoja ambayo itaonekana wakati wa utetezi.

Mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi hizo na kusema ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo ila baada ya notisi ya wakili wa utetezi,Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi itakapomaliza kusikilizwa mahakama kuu.

Hata hivyo, Lema hakuwepo mahakamani ambapo wakili wake alidai hati ya wito wa kutoka gerezani anakoshikiliwa kwa kukosa dhamana katika kesi nyingine za uchochezi,haikupelekwa gerezani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles